Make your own free website on Tripod.com
The Opulukwa Foundation
New Year Wish (2004)
Scholarships
Opulukwa ndani ya CCM
The Opulukwa Foundation
Uchambuzi na Hebron Mwakagenda
Chama Cha Mapinduzi (CCM)

ccm_emblem.gif

KARIBUNI WAPIGA KURA WANGU!

Utambulisho
Jina: Meshack Opulukwa
Kuzaliwa: 07/27/1967
Elimu: Shule ya Msingi Balili-Bunda; Shule ya Sekondari "O" Level-Bupandagila Secondary School (1988), Bariadi; "A" Level-Geita High School (1991). Baada ya kumaliza hii elimu ya awali, nilijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1993 hadi 1996 nilipohitimu shahada ya juu ya Sayansi ya Jamii-Ardhi na Mazingira. Mwaka huohuo 1996 nilianza kufanya kazi hapohapo Chuo Kikuu nikishughulika na uzazi salama wa mpango"Reproductive Health" kama meneja mradi hadi January 1997 niliapocha kazi na kuajiriwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (costech) . August 1998, nilienda Japan kusomea usimamizi na utunzaji wa mikoko katika kituo cha Okinawa, "management of mangove ecosystems" na baada ya kutoka huko nilijiunga na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine kusomea usimamizi  wa maliasili na kilimo endelevu, "management of natural resources for sustainable agriculture"
Mwaka 2000 nilihitimu masomo yangu toka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine na kurudi kwa mwajili wangu (costech). Mwaka 2001 nilienda Marekani kusomea uongozi katika taaluma ya, "Leadership and professional developement" katika Chuo Kikuu cha Purdue. Mwaka 2002 nilijiunga na Chuo Kikuu cha Hartford kilichopo Marekani kusomea shahada ya tatu PhD. "wildlife management" ambapo nategemea kuhitimu masomo yangu mwaka 2004 tayari kurudi nyumbani kuwafanyia kazi wananchi.
 
Siasa
Mwaka 2000 nilianza kujihusisha na siasa za Tanzania na niligombea Ubunge kupitia tiketi ya UDP katika jimbo la Meatu mkoani Shinyanga ambapo mgombea wa Chama Cha Mapinduzi-Mhe. Jeremiah Mulyambate Jisaba aliibuka kidedea. Matokeo ya uchaguzi yalikuwa kama ifuatavyo: CCM kura10,900, UDP-Meshack Opulukwa 10,500 na TLP- Ndugu Kabelele aliambulia kura 500. Kwa matokea hayo yamenitia nguvu sana kuendelea na shughuli za kisiasa na sasa ninaendelea na maandalizi kwa uchaguzi ujao kiti cha Ubunge jimbo la Meatu 2005. Baada ya uchaguzi mkuu, niliamua kurudi na CCM baada ya kuona kuwa vyama vya upinzani vilikuwa vimepoteza dira na uelekeo.
 
Shukrani
Nachukua fursa hii kuwashukuru sana wananchi wa Jimbo la Meatu wlioniunga mkono kwa dhati katika uchaguzi uliopita 2000 kwa kura nyingi. Napenda pia kuushukuru uongozi wa CCM mkoa wa Shinyanga kwa mapokezi makubwa na ya aina yake waliyonifanyia wakati wa kurejea kwangu "nyumbani" CCM. Shukurani nyingi zimwendee Katibu wa CCM (M), Katibu Msaidizi,  Mwenyeki wa Umoja wa Vijana Mkoa. Si rahisi kutaja mtu mmoja mmoja lakini nawashukuru sana wote kwa ujumla. Aidha naushukuru uongozi wa CCM wilaya ya Meatu kwa mapokezi ya aina yake pia. Shukurani za pekee ziwaendee, Mwenyekiti wa CCM (W), Katibu (W), Mkuu wa Wilaya, Kamanda wa Vijana, Afisa Usalama, Akina mama, Vijana na vikundi mbalimbali kama vile wasukuma matololi n.k.
Pia natoa shukurani zangu za dhati kwa waandishi wa habari kupitia magazeti ya Msanii Africa, Majira na Radio Free Africa kwa kazi nzuri ambayo wamekua wakiifanya hususani katika suala zima la kuandika habari zangu wakati wote wa kampeni za uchaguzi mkuu 2000 hadi kurejea kwangu CCM.

Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Habari za Tanzania

Mkono and Co. Advocates

Mfuko wa maendeleo
"The Opulukwa Foundation"

 

Kuanzishwa

 

Mfuko huu ulisnzishwa rasmi mwaka 2002 huko Marekani na Familia ya watoto wa marehemu mzee Jeremiah Opulukwa. Ndugu Meshack Opulukwa ndiye Katibu Mkuu Mtendaji wa mfuko huu.

Madhumuni

Madhumuni ya mfuko huu, pamoja na mambo mengine, ni kusaidia kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nyanja mbalimbali zikiwemo elimu, na kuwahamasisha wananchi kujihusisha katika kuandaa progmamu kwa ajili kujiletea maendeleo yao wenyewe. Mkazo mkubwa utatiwa katika nyanja ya elimu kwa vijana wanaohotimu elimu ya msingi na sekondari ili waweze kufikia ngazi ya chuo kikuu.

Matumizi ya fedha za mfuko

Hadi sasa mfuko umefanikiwa kupata dola za kimarekani $ 19,000 (shs milioni 19 za Tanzania) kutoka kwa wafadhili. Awamu ya kwanza ya matumizi ya fedha hizi ni kusomesha watoto wawili kila mwaka kwenda kidato cha kwanza ambao wazazi wao hawana uwezo wa kuwapeleka shule pia kulingana na uwezo wao kimasomo. Halmashauri ya wilaya ya Meatu itasimamia upatikanaji wa wanafunzi hao ikishirikiana na katibu mkuu mtendaji wa The Opulukwa Foundation. Mfuko utaendelea kuwaghalimia hadi hapo watakapohitimu masomo yao bila kujali watakuwa wamefikia ngazi gani ama, kidato cha tano, sita au chuo kikuu. Wanafunzi hao wataanza kulipiwa kuanzia January 2005.

Awamu ya pili itaanza Octoba 2005 kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu au misaada kwa vikundi mbalimbali vikiwemo, akina mama, vijana, wazee, na wasiojiweza. Mikopo hiyo italenga zaidi kununulia vitedea kazi kama vile vyerehani, nyavu za uvuvi wa samaki, matoroli ya kisasa na biashara ndogondogo.

Muda wa mfuko huu ni miaka mitano ambayo itaishia 2010. Baada ya hapo awamu ya tatu itaanza kutegemeana na mahitaji ya wananchi wa jimbo. Hata hivyo, upatikanaji wa gari la kufuatilia ng'ombe wanaoibwa pamoja na gari la kubebea wagonjwa ni miongoni mwa mambo yatakayopewa kipaumbele katika awamu ya tatu. Makao makuu ya mfuko huu yatakuwa Mwanhuzi-Meatu.

(c)Copyright 2003, All Rights Reserved
 
kwa mawasiliano, unaweza kunipata kupitia:
 
2130 NW 31st Ave, Apt K11
Gainesville, FL 32605
Tel.(352) 378-3665